"NILIYE MFUMANIA NA MPENZI WANGU KANIANGUSHIA KIPIGO CHA MBWA"
Nina mpenzi wangu ambaye yuko chuo
fulani hapa Dar lakini
kutokana na maamuzi yetu tuliamua aishi mtaani
badala ya Hostel. Huyu msichana nilianza nae mahusiano kwa kipindi
kirefu sana na hata tumefikia kuvalishana pete na nyumbani kwao
nafahamika pia.
Kutokana na shughuli zangu nyingi kua mikoani hua tunakutana kwa baadhi ya wikiendi tu ninapokuja hapa Dar.
Basi Ijumaa hii nikaona sio vibaya
kum-surprise my wife to be. Nikatoka zangu mkoani na shauku ya kujiandaa
kwenda kwa P-square na mamaa.
Nilipofika pale Geto kwake hali
sikuielewa. Nikaona sio mbaya kubisha hodi. Niligonga kidogo tu sauti
yenye hasira na mikwaruzo ikatoka ndani. "Wewe Nani"???
Nikajibu kwa kujiamini nikijua wako discussion na wenzake.. "Mimi ni Edwin"
Ndani nikasikia kama wanabishana kidogo.
Ghafla jamaa akafungua mlango na
kuniuliza huku amekasirika wewe nani? Nikajibu kwa kujiamini. "Kama
Grace yupo ndani muulize Edwin ni nani?"
Basi Grace alipoulizwa akakana
kunifahamu. Hapo jamaa akaanza kunishushia kipigo. Kutokana na mwili
mdogo nilionao jamaa alinipga kwa kweli huku akitishia kunipigia kelele
za mwizi.
Basi baada ya pale nikaenda hospital
kupata matibabu. Nikaamua kumtaarifu mama yake Grace. Mama Grace
alishangaa sana na kudai mbona Grace alimtaarifu tumeachana kwa Mwezi
sasa?
Nikachanganyikiwa zaidi. Nilipopeleleza
zaidi kwa rafiki yake mmoja, nikagundua jamaa ndio anamgharamia Grace
kila kitu na kias nilichotoa kwa Grace ilikua hela ya chumvi tu..
Hapa nilipo nina maplasta usoni na sehemu nyingine.
Nisaidieni nichukue hatua Gani kisheria
juu ya huyu jamaa? Je akisema nilitaka kuiba nitajitetea vipi? Ushauri
wenu ni muhimu sana
Note
Nimetumia majina ya kweli ili kama Grace
yupo humu ndani ujumbe umfikie na ajue ameniumiza sana moyoni kwa
usaliti aliouonyesha mchana kweupe.
Asanten
Source: Udaku Specially
No comments:
Post a Comment