WOLPER AWAONYA MABINTI WANAOMSHOBOKEA MPENZI WAKE

Jacqueline Wolper.
Na Mayasa Mariwata
Jacqueline Wolper amesema kuwa, ana imani
kubwa na mpenzi wake wa sasa aliyemtambulisha kwa
jina la G Modo
akiamini atampoza machungu aliyoyapata kutoka kwa mpenzi wake wa zamani,
Abdallah Mtoro ‘Dallas’ huku akiwatahadharisha mashosti zake kutoleta
shobo (kuwa mbali naye). Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Wolper alisema anafikia hatua ya kusema hayo kwa kuwa muda mfupi aliokuwa naye amegundua ni mwanaume anayejitambua na anayeheshimu mapenzi ila akawataka mashosti zake kutomsogelea.
“Tangu niwe na huyu kijana nimekuwa ni mwenye furaha kubwa, nasahau hata yale machungu niliyopata kwa mpenzi wangu wa zamani. Lakini najua wapo wanaomtolea macho, tusitafutane ubaya, kila mtu na maisha yake,” alisema Wolper.
No comments:
Post a Comment