MADAM RITA ASEMA WANAUME WALIM.......AKIWA MDOGO
Madam Rita ameamua kuweka wazi baadhi ya mambo yaliyomsibu akiwa bado msichana .
Hiki ndicho alichokiandika kupitia account yake ya Facebook:
"Jambo mmoja msilofahamu kuhusu mimi....
Nilipata
ujauzito nikiwa na umri mdogo sana. Kwa jamii yetu inayotuzunguka,
ukizaa katika umri mdogo, watu huwa wanakunyanyapaa, hukuona haufai kuwa
katika jamii na hata kukuhukumu. Kwa umri ule niliona ni kama hamna
tena maisha kwangu lakini sikukata tamaa na leo hii ujasiri wangu na
kitu kinachonipa msukumo wa maisha hadi kufika hapa nilipo ni hicho
kilichonikuta nikiwa na umri mdogo."
"Kukataa tamaa isiwe ndio chaguo lako la kwanza'Alisisitiza Madam Rita.
No comments:
Post a Comment