
Menina Atick.
MWANAMUZIKI aliyeibukia kwenye Shindano la Epiq Bongo
Star Search mwaka
2012, Menina Atick; amesema licha ya kusikia na kubaini kuwepo kwa baadhi ya wanaume
wenye nafasi kwenye ‘game’ la muziki ambao wamekubuhu kuomba rushwa ya ngono kwa
wasanii wa kike ili wawatoe, yeye atakomaa na anaamini atasimama.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Menina ambaye sasa anasumbua na
wimbo wake wa Shaghala Baghala alisema anachoamini ni kwamba msanii wa
kike mwenye kipaji hata asipotoa rushwa ya ngono, nafasi ya kung’ara
anayo, hivyo yeye atakuwa mfano kwa wengine.
“Mimi…nitoe rushwa ya ngono ili nitoke, mh…kwa kweli hiyo
haiwezekani, najiamini na sitakubali kuutumia mwili wangu kwa kugawa
penzi ili nisimame kwenye muziki, kwanza nitatembea na wangapi,” alihoji
msanii huyo.
Source: GPL
No comments:
Post a Comment