
Duniani kuna mambo na vijimambo, bibi na bwana harusi
waliojikita katika kutetea haki za kupiga picha uchi, Gypsy Taub na mkewe Jaymz Smith waishio San Francisco wamejikuta wakilia honeymoon yao lupango baada ya kuvua nguo zao zote wakati wakifunga ndoa.
waliojikita katika kutetea haki za kupiga picha uchi, Gypsy Taub na mkewe Jaymz Smith waishio San Francisco wamejikuta wakilia honeymoon yao lupango baada ya kuvua nguo zao zote wakati wakifunga ndoa.
Kwa
mujibu wa ‘The San Francisco Chronicle, bibi harusi alifika katika eneo
la tukio akiwa amevaa nguo kama kawaida lakini alizivua zote ghafla
na kubaki mtupu kama alivyozaliwa kisha akapaza sauti, “hii ni kwa ajili
ya kupinga sheria zanazokataza kuwa mtupu kwa namna ambayo imekuwa
katika ndoa.”
Naye
mfungishaji ndoa ambaye sio kiongozi wa dini yeyote, alisema “najua
watu wa San Francisco wako nyuma yangu,” na kisha kuwaambia wana ndoa
hao, “sasa mnaweza ku-kiss na kufanya ngono.”
Gazeti
hilo limeripoti kuwa tukio hilo lilifanyika hadharani karibu na makazi
ya watu ambapo wanawake wengi na watoto walikuwa wakipita eneo hilo.
Baada
ya shangwe za ndoa hiyo, maharusi walichukuliwa na gari la polisi na
kupelekwa panapohusika, na ripoti zinasema walifunguliwa mashitaka kwa
kosa la kujiachia watupu hadharani.
Hata hivyo wawili hao waliachiwa baadae huku tarehe za honeymoon zikiwa zimeishia selo.
Lakini waliporudi uraiani waliliambia The San Francisco Chronicle kuwa ndoa yao ilikuwa nzuri na ya kufurahisha.
“It was fantastic…it surpassed all my expectations. It was just an awesome party.” Bwana harusi Taub alijigamba.
No comments:
Post a Comment